SME
Mkopo wetu wa SME unalenga biashara binafsi, biashara ndogo na za kati zinazofanya kazi ndani ya majengo maalum yaliyosajiliwa. Kiasi cha mkopo kinaweza kuwa kati ya 50,000 hadi 50,000,000 kulingana na ustahiki wako. Tunazingatia mtaji wa biashara na utendaji wa biashara yako kutathmini kiasi cha mkopo. Mmoja wa maafisa wetu wenye uzoefu wa mikopo atakagua maombi yako na mahitaji ya biashara yako dhidi ya hatari na kisha kukushauri ipasavyo.
Mahitaji ya mikopo ya SME:
- Lazima uwe unaendesha biashara halali kwa kipindi kisichopungua mwaka mwaka mmoja.
- Kuendesha biashara katika Jengo/eneo kwa angalau miezi 6 katika eneo la sasa.
- Mkataba wa ukodishwaji wa pango/eneo la biashara unapaswa uwe ndani ya kipindi cha mkataba wa mkopo.
- Lazima uwe raia wa Tanzania na mwenye umri wa miaka 18 - 65 wakati wa mkopo wa kwanza.
- Dhamana inayokubalika kulinda mkopo
- Lazima uwe na biashara yenye mtiririko wa fedha unaotabirika.
