Mkopo kwa Dhamana ya Kadi ya Gari
Mkopo wetu wa LBF unalenga wafanyabiashara, wafanyakazi wa sekta ya umma na binafsi ambao watapata mkopo kulingana na mtiririko wao wa fedha huku gari yao ikiwa dhamana. Kiasi cha mkopo kinaweza kuwa kati ya 2,000,000 hadi 30,000,000 Tsh kulingana na mtiririko wako wa fedha. Tutazingatia utendaji wa biashara yako au mishahara ya miezi 3. Mmoja wa maafisa wetu wenye uzoefu wa mikopo atakagua maombi yako na mahitaji ya biashara yako dhidi ya athari na kisha kukushauri ipasavyo. Bidhaa hii sasa inapatikana katika mikoa yetu minne pekee ambayo ni MOSHI, ARUSHA, DODOMA na DAR ES SALAAM.
Ifuatayo ni sifa na mahitaji ya mikopo ya LBF:
- Lazima umiliki gari.
- Bima inaweza kuwa ndogo au kubwa kulingana na kiasi cha mkopo
- Lazima uwe na Kitambulisho cha Taifa na leseni ya udereva.
- Barua ya utambulisho kutoka Serikali ya Mtaa
- Taarifa ya benki ya angalau miezi 6
- Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi – TIN
- Kitambulisho cha Taifa cha mdhamini.
- Leseni ya Biashara/Kivuli cha Mkataba wa Ajira
- Picha 2 za Pasipoti
- Kwa mfanyakazi, lazima awe na slipu ya mshahara ya angalau miezi 3 na katika hali hii na Kivuli cha kitambulisho cha kazi.
