Mikopo ya Biashara
Mkopo wetu wa SME unalenga biashara binafsi, biashara ndogo na za kati ambazo zinafanya kazi ndani ya majengo rasmi yaliyowekwa. Kiasi cha mkopo kinaweza kuwa kati ya Tsh 50,000 hadi 50,000,000 kulingana na ustahiki wako. Tutazingatia utendaji wa biashara yako au SME ili kutathmini kiasi. Mmoja wa maafisa wetu wa mikopo wenye uzoefu atatathmini maombi yako na mahitaji ya biashara dhidi ya hatari na kisha kukushauri ipasavyo.
Mahitaji ya mikopo ya SME:
- Lazima uwe unaendesha biashara halali kwa kipindi kisichopungua mwaka mwaka mmoja.
- Kuendesha biashara katika Jengo/eneo kwa angalau miezi 6 katika eneo la sasa.
- Mkataba wa ukodishwaji wa pango/eneo la biashara unapaswa uwe ndani ya kipindi cha mkataba wa mkopo.
- Lazima uwe raia wa Tanzania na mwenye umri wa miaka 18 - 65 wakati wa mkopo wa kwanza.
- Dhamana inayokubalika kulinda mkopo
- Lazima uwe na biashara yenye mtiririko wa fedha unaotabirika.
